Hujambo,
Kwa heshima kuu, ningependa kuweja ombi la kupewa nafasi ya kufanya kazi ya kutafsiri kutoka lugha ya Kiingereza, kwa Kiswahil, kama mlivyo tangaza kwenye wovuti wa freelancer.
Mimi ni mkenya asilia, na nina uwezo wa kusoma, kuandika na kusema kiswahili sanifu, bila shida zozote. Nina ujuzi wa kufanya kazi kwa lugha ya kiswahili, sio kwamba tu nilisoma shuleni na kwenye chuo, lakini miaka kadhaa iliyopita, nilifanya kazi kwenye sehemu ya pwani ya kenya, huko Lamu. Wakati huo, nilifanya kazi ya mawasiliano, kwa lugha ya kimombo, "Communications Officer". Wakati wa kazi yangu, nilikuwa na wajibu wa kuwasiliana na wenyeji wa vijiji vya kisiwa cha Lamu, na wakati mwingi, niliendeleza kazi yangu kwa lugha ya kiswahili. Nilikuwa pia na jukumu la kutafsiri nyaraka tofauti kutoka Kiingereza na kiswahili hasa wakati wa kufanya kazi na wenyeji wa Lamu.
Ninatumai kwamba ombi langu litapata kujibiwa, na ninatumaini kupata kazi hii.
Asante sana na ninabaki ha hamu ya kupotea majibu yako.
Ni mimi wako,
Lilian